... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Maisha Yako Hapo Ulipo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 2:8,9 Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, utukufu wa Bwana ukawang’aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.

Listen to the radio broadcast of

Maisha Yako Hapo Ulipo


Download audio file

Duniani kote, katika jiji, miji, vijiji na mashambani, hata jangwani, maisha yanaendelea tu.  Tukio la ajabu-ajabu linaweza likatokea sehemu moja, lakini pengine pote, shughuli zinaendelea kama kawaida.

Kupitia miaka isiyo michache nimetembelea nchi nyingi.  Kuanzia Visakhapatnam huko India hadi Kigoma, Tanzania, kutoka Vienna hadi Vancouver, kutoka … lakini nadhani mifano hii inatosha.  Sasa, ninapofika nchini fulani na kuanza kutembea barabarani, inanishangaza kila mara jinsi maisha ya pale yanaendelea kama kawaida tu.  Ulimwenguni kote, watu wanaishi katika tamaduni mbali mbali, wakiwa na desturi tofauti-tofauti katika mavazi, vyakula, mwonekano, tofauti ya mazingira hata harufu na kelele tofauti. 

Halafu maisha ya hapa, sehemu fulani, haijalishi hata kidogo maisha yanayoendelea huko.  Maisha ya hapa kwetu yanaendelea bila kujali habari ya maisha huko kwenu.  Ndivyo ilivyokuwa kwa jamaa hawa ambao tunaenda kusikia habari zao: 

Luka 2:8  Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku.   

Walikuwa wanaendelea na kazi zao kama kawaida.  Lakini ghafla … 

Luka 2:9  Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, utukufu wa Bwana ukawang’aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. 

Katoto kalikuwa kamepenyeza ulimwenguni usiku ule katika kijiji kidogo kiitwacho Bethlehemu; katika zizi dogo kwa sababu hapakuwa na nafasi kwenye gesti.  Lakini KUMBE!  Kuzaliwa kwake kusikojulikana kwa mtoto aitwaye Yesu (ilikuwa jina lililotumika sana wakati ule) kuliwashtua wale wachungaji kwa jinsi ya ajabu sana! 

Tukio lile la ajabu la Yesu, wakati Mungu akifanyika mwanadamu ili atuokoe na hali yetu ya asili, tukio lile limeingilia maswala ya ulimwengu mzima tangu wakati ule hadi leo. 

Acha Yesu akatize na kuingilia ratiba maishani mwako! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.