... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Maisha Yako Mapya Yanatakiwa Yawe …..

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wakolosai 3:12 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole uvumilivu.

Listen to the radio broadcast of

Maisha Yako Mapya Yanatakiwa Yawe …..


Download audio file

Pale mambo hayaendi kama ulivyotazamia, pale watu hawaendi sambamba na wewe ni rahisi kuwalaumu au kulaumu mazingira yako na hata kumlaumu Mungu.  Ndivyo tulivyo kiasili. 

Tunaishi katika ulimwengu ambao watu wanazidi kulaumu wengine kwa ajili ya matatizo yao, wakilaumu serikali, uchumi, au…kingine chochote kile wanachoona mbele yao. 

Lakini kujiangalia wenyewe kama kwa kioo, na kuwajibika na hisia zao, mawazo yao na mienendo yao….wala!  Hawataki kuwajibika hata kidogo. Kwanini kukubali kuwajibika wakati ni rahisi kulaumu mtu mwingine?  Sisi sote tumewahi kuwa na mtazamo kama huo – na hata katikati ya watu wa Mungu, bado watu wanaendelea kulaumiana na yawezekana isije isha. 

Juzi nilikuwa nimechoka sana. Baada ya kazi, tulipata cha pamoja na watu wengine, nikifikiri itachukua muda mfupi tu, lakini waliendelea kukaa hatimaye nilianza kuchoshwa na kuchikizwa nao. 

Sasa ikitokea hivyo, na huwa haina budi kutokea, mtu atafanyaje? 

Wakolosai 3:12  Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole uvumilivu. 

Nikitumia mfano ambao nimetoka kuutaja sasa hivi, inabidi nitekeleze andiko hili kwa sababu upendo wa Mungu umetutengea maisha mapya, ili tubadilike, tukaishi maisha mapya na kuwahurumia wengine. 

Wito huo unafananaje?  jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole uvumilivu.  

Kama vile mchungaji akiwa mwanatheolojia na mfia dini pia, Dietrich Bonhoeffer aliwahi kusema:  Kumjua Mungu ni kubadilika! 

Kumbukumbu:  Wajibika! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.